MALAYA MZOEFU..05
Mtunzi: JONS JONAS

Msimuliaji:CLIFF DAVIS

WhstsApp:0613 321 991


Kabla sijaanza kukusimulia simulizi hii ya Malaya mzoefu sehemu ya tano, ningependa kukukumbusha jambo muhimu sana. Tafadhali hakikisha unasubscribe kwenye chaneli hii Ya Simulizi Extra, ili uwe wa kwanza kupata muendelezo wa simulizi hii pamoja na simulizi nyingine za kuvutia. Pia, usisahau kulike na kuacha maoni yako; maoni yako ni muhimu sana katika kutusaidia kuboresha simulizi zetu na kuhakikisha kuwa zinaendelea kukufurahisha. Kwa kufanya hivyo, utakuwa umetisha kinomanoma!

Sasa bila kupoteza muda, wacha nikupeleke moja kwa moja kwenye simulizi yetu ya leo, inayomhusu mrembo Tina, ambaye alitumia mwili wake  barabara kujifurahisha.

Mimi ni mr.story Cliff Davis, na ni faraja yangu kubwa kukukaribisha kwenye safari hii ya kusisimua. Twende tukaendelee na simulizi hii..

 

::Tuliishia pale ambapo tina amepewa lift na kaka yake jerry na tayari wapo kwenye gari na safari ya kuelekea magomeni inaendelea huku utambulisho wao ukiendelea na tina kashamdanganya kaka yake jeery kuwa yeye ni jirani yao na pale alipo anasafari ya kuelekea kariakoo….we unafikili nini kinajili twende pamoja……

:: NJia nzima nilikuwa nikimwangalia kwa jicho la kuibia ibia huku matamanio yangu yakichukuwa nafasi yake, mpaka alipofika magomeni pale usalama, akapaki gari yake pembeni, “…mie naishi hapo kituo cha mbele ‘magomeni mwembe chai’ lakini natumai utapanda daladala pale za kwenda kariakoo..” “..wala usijari, kuna kitu naenda kununua mara moja halafu nakurudi kwangu ‘Ilala’..” Nilimdanganya tena kwa kujiamini, ile hali ya ujasiri nilikuwa nayo bila hata kuwa na mshipa wa aibu.. “..amh nimesahau kujitambulisha, mie naitwa Grace ni mfanyakazi mwenzake na Jerry..” “..ahaa, ni vizuri binti, mimi kama unavyomwona mwanangu hapa pembeni, naitwa Baba Latifah au ukipenda niite Ustadhi Juma…” “…ok, usijali labda kwa hapa sina ‘business card’ zimeniishia, labda ungenipa namba yako ya simu na mimi nikupe yangu..” “..ooh, wala usijari Grace,..Alinipa namba yake ya simu na mimi Niliichukuwa nakumpa namba yangu huku nikiondoka na uhakika wa hali ya juu mpaka kwenye daladala ziendazo posta na siyo tena kariakoo kama nilivyokuwa nimemdanganya hapo awali, “..na hivi leo sijaingia darasani, lakini Aisha atanielekeza walichofundishwa leo..” Niliendelea kuongea mwenyewe huku nikiwa ndani ya daladala maeneo ya ‘fire’ karibu na kituo cha ‘akiba’ ambapo ndipo ninaposhukia kwenda chuoni kwetu ‘cbe’. Nilipofika tu ‘hostel’ breki ya kwanza ilikuwa nikuvua ile mi nguo ya baibui kwani ilikuwa imenijazia joto sana, “..shosti kwa mishemishe, hata hutulii..?” Alikuwa Aisha akiongea na mimi. “..nitulie wapi wakati mjini kuna mambo mengi! Haya embu niambie mlichofundishwa leo..?” “..leo tumefundishwa somo moja tu..” “..lipi hilo” “..Entreprenuer..” “..na mwalimu wa ‘Law’ hakuingia..?” “..yule katuambia mpaka wiki ijayo hivyo tujiandae kwa ‘test’ kutoka kwake..” * Usiku wote akili ilikuwa ikimuwaza Baba Latifah, kila muda nilipotaka kumtumia meseji nilikuwa nasita nakuhisi huenda akaipokea mke wake nikaharibu kila kitu nakumkosa kabisa, hivyo nikajilalia zangu mpaka asubuhi.. Nilikuwa nakipindi asubuhi hivyo nilitumia masaa mawili nikawa sina tena kipindi, “..kwa muda huu kama hayupo ofisini sijui..” Niliichukuwa simu yangu nakumpigia baba Latifah, lakini iliita tu nakukatwa hapo hapo, Woga ulianza kuchukuwa nafasi yake katika mwili wangu huku akili ikinituma kuwa huenda ameshajua mchezo wote ninaoufanyaga.. Nikiwa ndani ya dimbwi la mawazo kwa muda mfupi mara simu yangu ikaita, harakaharaka nikaangalia jina lilikuwa ni baba Latifah, nikaipokea kwa pozi na tabasamu zito, “..hallow,” “..yeah, nani Grace?” “..ndio unaongea na Grace..” “..nisamehe binti, nilikuwa naendesha gari ndio maana niliikata simu yako lakini usijari, nimeshafika na kwasasa nipo hapa hapa ofisini kwenu..” “..uko wapi baba Latifah..?”

Niko hapa ‘aiport’ unapofanyia kazi na mdogo wangu Jerry, na nimekuja kufuatilia pesa zake kwa ajili ya matibabu, wewe uko kwa wapi..?” Nilijihisi mdogo ghafla kama kidonge cha ‘piriton’ huku nikiamini kwa asilimia zote nitakuwa nimeshaharibu haswa akiulizia jina la Grace akaambiwa hamna jina hilo nitakuwa simpati tena. Hapo hapo akili yangu ikachemka ghafla nakupata wazo nakumjibu.. “..nimetoka ofisini na nipo posta kuna bidhaa tumeleta hivyo kwa leo sintoweza kurudi ofisini mpaka kesho, lakini nahitaji kukuona leo jioni kuna vitu ninavyo nataka umpelekee mgonjwa ‘Jerry’ mie nimebanwa sana..” “..wala usijari binti, wewe niambie nikukute wapi..?” “…kwa sababu nitakuwepo posta mpaka jioni sana, nitakutafuta kwenye mida ya saa kumi na mbili, samahani kwa usumbufu lakini..” “..kuwa na amani kabisa binti yangu..” Nilimaliza kuongea na simu huku furaha kubwa nikiwa nayo, nikatafuta nguo ya kuvaa ambayo itaendana na zile za wafanyakazi wa ‘airport’ Hatimaye nikapata kisketi cha bluu na shati jeupe lililonipana na nikachukuwa kikoti cha Aisha cha bluu nachenyewe chakubana na kisha nikafunga funga mtandio wa bluu ndio ikawa kama tai.. Saa kumi na mbili kasoro nilikuwa nipo ‘Subway’ posta nikiwa nimeifunga kanga yangu ndani ya karatasi la kuhifadhia zawadi na juu yake nikiandika maneno ‘Get well soon Jerry’ (ugua pole Jerry) huku nikimsubiri baba Latifah… Nilimpigia simu kujua amefika wapi, “..hallow, nipo hapa ‘subway’ posta nakusubiri..” “..nami nakaribia nipe dakika kama kumi..” Sikusubiria sana akawa ameshafika, nilijifanya ninaharaka sana na nimechoka na mizunguko toka asubuhi nilipotoka na wenzangu kumbe wote uongo.. “…pole sana na kazi, ndio majukumu yalivyo..” “..chukuwa hii ni zawadi kwa Jerry ataifurahia sana akiifungua na utamwambia kuwa imetoka kwa wafanyakazi wenzake..” Aliichukuwa, “..ok, kwakuwa umechoka sana wacha nikusogeze mpaka karibia na kwako, uliniambia unaishi wapi tena..?” “..Ilala boma..” Giza lilikuwa limeshatanda, tukaingia ndani ya gari lake, Nikamuwahi kabla hajaliwasha nikamshika mkono, akashangaa..!! “…najua umeoa na una mtoto, ningependa leo nikucheleweshe kidoogo kurudi kwako..” Baba Latifah alikaa kimya huku akihema juu, hapo hapo nikavua kikoti changu nakusingizia joto.. Akiwa bado ananishangaa nikaanza kuvua vishikizo vya shati huku kisketi nikikipandisha kwa juu nakuachia mapaja wazi… Kigugumizi kiliendelea kumshika baba Latifah, “..vipi binti..? Mbona sikuelewi..?” “..hunielewi..? Mwenzio nasikia joto kweli hapa, yaani hili joto la Dar balaa kweli..” Niliendelea kusingizia joto huku nikitoa tabasamu feki kwa baba Latifah.. “..lakini gari yangu ina A/c si ungeniambia tu nikuwashie..” “..dah.. Nilijisahau, lakini nilivyofanya kwani ni vibaya..?” Hakunijibu zaidi yakuliwasha gari, niliuwahi ufunguo kabla hajaondoka nikalizima kisha nikatoa ufunguo wa gari nakumtolea macho baba Latifah. “..Samahani kwa kukufanyia hivi ila nakuomba unisaidie kitu kimoja tu..” “..eh..! kitu gani hicho..?” Nikachukuwa pochi yangu nakuchomoa shilingi elfu mbili. “..samahani sana, unajua mimi ni mtoto wakike kama walivyo wengine, na hali hii imenitokea ghafla..” Baba Latifah alionesha kushtuka huku akihema juu juu. “..sijakuelewa, unamaanisha nini tena..” “..nimeingia katika mwezi ghafla (na bleed), na sijatembea hata na ‘pedi’ nakuomba ukanichukulie pale dukani, samahani sana mzee wangu, kwani hapa nilipo nahisi damu zinanimwagika na nimeshajichafua ” Baba Latifah alinielewa, hakuchukuwa pesa yangu, alichokifanya alishuka kwenye gari nakuelekea dukani. Ndani ya muda mchache alikuwa amesharudi huku mkononi mwake akiwa ameshikilia mfuko. Alinipa nikaufungua nakutoa ‘pedi’ moja kisha.. “..samahani tena..?” “..kwanini..?” “..siwezi kubadilisha pedi kwani nimechafuka sana, nahitaji nijisafishe kwanza, pili sijatembea na nguo ya ndani ya akiba..” “..kwa hapo sijui hata nitakusaidiaje binti..” Baba Latifah akiwa bado anajifikiria huku ananiangalia, na ukizingatia tulikuwa ndani ya gari lenye vioo vyeusi huku nje giza likiwa limeshatanda. Niliivua ile nguo yangu ya ndani kisha nikafungua kioo nakuitupa kwa nje, lakini muda huo.. “…najitahidi kujizuia lakini mie mtoto wakike tena niliyeumbwa kwa aibu, nisamehe kwa kilichonitokea..” “..hilo tu..! Wala usijari kabisa..” “..hivi kwa mfano nikawa mke wako wa pili, si utakubali..?” Nilianza maswali yakumtega baba Latifah kabla hajaliwasha tena gari.. “…ni kweli hata dini yetu inaruhusu, ila kwa wewe bado mdogo sana, na wala bado sijalifikiria hilo..” Nilimwangalia kwa jicho la hasira tena ile ya ghafla huku nikiubenua mdomo wangu.. “..Ananiona mdogo hee, na leo ataniona mkubwa sasa..” Nilijisemea kimya kimya huku nikiuchukuwa mkono wangu mpaka kifuani mwake nakuanza kumshika manywele yake ya kifuani bila ruhusa yake, kitendo cha kukaa kimya bila kuniongelesha chochote kilichochea zaidi hisia zangu nakuusogeza uso wangu mpaka nikakutana na uso wake, nilimshuhudia baba latifa uzalendo ukimshinda taratibu akaanza kupapasa maungo yangu “..baba Latifah, mie bado binti mdogo tena sana, najishangaa nimepatwa na hisia ghafla, najua hii yote inatokana na hii ‘period’.. Nakuomba uwashe gari unipeleke kwangu Ilala..” baba Latifah hakunielewa wala kunijibu chochote, nikamwita tena.. “..baba Latifah, naongea na wewe..?” Bado alinitazama tu, nilichokifanya, nikavua nguo zangu zote nikabaki kama nilivyozaliwa muda wote huo baba latifa alikuwa akiniangalia tu huku akihema juu juu kisha nikikaa juu ya mapaja ya baba Latifah.. “..Grace utanichafua na damu zako binti, kwanza si una ‘bleed’ wewe..?” nilicheka kwa muda kisha nikazibana nywele zangu vizuri nakumjibu.. “..hapana bwana baba Latifah, nilifanya vile kujiweka sawa tu, si unajua sisi wasichana tukianza kujihisi hali kama ile tunatakiwa tuwe na ‘pedi’ karibu..” “..kwa hiyo unamaanisha hau ‘bleed’..?” “..ndio manake, au kama unabisha washa taa aushika uone kama mimi na ‘bleed’..”Baba latifa kweli akasogeza mkono na kukagua ili hajiakikishie “..haya umeniamini sasa..?” hakunijibu lolote Zaidi ya kuniangalia tu

:: Tayari baba Latifah alikuwa kwenye himaya yangu huku akiwa si mtu wakujiamini amini kwa kile nilichomfanyia.. nakuambia hakika tuliweza kufanya mapenzi ndani ya gari tena kwa uhuru Zaidi ile tuna maliza tu mala tuasikia hodi ikipigwa kwenye vioo vya gari… Baba Latifah alionesha kushangaa sana, alinisukuma pembeni kisha akavaa nguo zake haraka haraka nami nikavaa hivyo hivyo japokuwa tayari nguo yangu ya ndani nilikuwa nimeshaitupa nje kabisa.. Ndani ya muda mchache Baba Latifah alinitolea macho kisha akabonyeza kidude cha kushusha kioo ili kumjua ni nani.. “..ahaa hujambo John..” “..sijambo shikamoo kaka..” Nilikuwa nimeshagundua kuwa alikuwa ni John tena yule niliyempa ukimwi na kwa muda huu nilibaki ndani ya gari huku Baba Latifah akishuka nakuongea naye.. Nilitega sikio huku nikiwasikiliza kwa mbaali.. “..vipi unafanyaje huku John..” “..bro nilikuja mara moja na rafiki yangu tunayesoma naye hapo ‘Ifm’ lakini nimeshaachana naye baada ya kuona gari lako umepaki maeneo haya vipi bro Jerry anaendeleaje..?” John alizidisha story na Baba Latifah hadi woga ukaniingia nakuona hapa kama nitaendelea kuwasikiliza hawachelewi kuingia ndani ya gari tukaondoka wote na nitakuwa nimeshaumbuka. Nilichokifanya niliiacha ile zawadi ya Jerry  kisha nikavishika viatu vyangu mikononi nakufungua mlango wa pili yake taaaratibu nikinyata huku nikiwaacha wakiendelea na maongezi.. “..watajuana tu ndo nimeshawaachia, mie ndio Tina sifi na mmoja na mwaka huu hata nikifa nahakikisha ukoo wao wote unanifuata kaburini..” Niliendelea kujisemea mwenyewe huku nikikatiza mitaa ya posta nakwenda mpaka ‘cbe’ kwa mguu kwani hakukuwa mbali. Nikiwa bado nipo njiani huku nimeshavalia viatu vyangu japokuwa nywele zilikuwa zimenivurugika hilo wala sikulijari mtoto wakike mie, mara ghafla simu yangu ikaita, nikaitoa kwenye pochi haraka haraka huku nikiangalia jina. Alikuwa ni John tena John yule niliyempa ukimwi pale kinondoni kwake, nikaipokea huku nikiongea kwa sauti ya taaratibu, “…hallow..!” “..hivi we mwanamke? Umeniambukiza ukimwi ukaona haitoshi na sasa umeamia kwa kaka yangu si ndio..?” “..hiyo ndio salamu, na huyo kaka yako sikumlazimisa alinifuata mwenyewe hapo unapopaona..” “..embu ona, ana familia inayomtegemea na hapa alipo ameniambia alikuwa na mdada hamuoni humu ndani, nilivyomonesha namba yako ya simu akapata presha ya ghafla, ona sasa unamuua pumbavu zako…” “..wapumbavu ni wewe Jerry na huyo sijui ndo kaka yenu mkubwa sijui ndo baba Latifah, na tena msubiri kama sijaja kwenye msiba wenu mtakuja kwenye msiba wangu..” “..unasemaje..?” “..kama ulivyosikia..” “..nilishakwambia na narudia kukwambia ama zangu ama zako nikikushika nahakikisha nakishona kwa sindano hicho kinanii chako unachowaambukiza watu wasio na hatia..” Hasira za ghafla zilinipanda nikaikata ile simu nakuizima hapo hapo kisha nikaidumbukiza kwenye kipochi changu nakuendelea na safari yangu yakurudi chuoni.. Nilipofika tu Aisha rafiki yangu alinipokea kwa fujo zote, “..niambie Tina wangu wa ukwee..! Ehh vipi tena shosti mbona leo umepooza hivyo..?” “..hamna wala hata sijisikii chochote, nimeamua tu niwe mpole, kwani hupendi..?” “..hee..? Makubwa, haya ndio ujiandae hivyo leo tunaenda muziki, tena nipo na shemeji yako ambaye hata humjui..” Nilibaki namtolea tu Aisha macho akiendelea kuongea kwani yote yalikuwa yanapitia sikio la huku nakutokea upande wa pili.. “..jamani Tina, si ujiandae twende wote na hivi leo ‘club bills’ wasichana bure..” “..Aisha..? Tungeenda ila akili yangu haiko sawa kabisa, ila kama utakubali nipumzike kama nusu saa ndio twende sawa tutaenda..” Aisha alinielewa, kwa uchovu nakulegea kwa mawazo yalionitawala kichwani mwangu nililala hivyo hivyo na nguo nilizokuwa nazo bila hata yakwenda kujisafisha.. Baada ya kama lisaa zima niliamshwa na rafiki yangu Lucy.. “..jamani bado nina usingizi mbona tunakatishana, haya huyo Aisha yuko wapi..?” “…yupo nje anaongea na bwana wake, na amenipigia simu nikuamshe ujiandae kisha tumfuate mpaka alipo huko nje..” Kwa jinsi nilivyonapenda starehe Tina miimi, haraka haraka niliingia bafuni nakuoga nilipotoka nilivaa kipensi changu kilichoachia mapaja yote wazi huku juu nikiwa na kiblauzi kilichoshikilia matiti tu, huku tumbo lote likiwa wazi nikaongozana na Lucy huku tukitoka nje.. “..haya we Lucy yuko wapi sasa huyo Aisha..? Na kama ametuachaaa…?” Niliongea kwa hasira baada ya kutoka nje nakuwakuta hawapo. Nikampigia Aisha simu.. “..hee Aisha mko kwa wapi..?” Simu yake ilipokelewa tu lakini haongei zaidi ya kusikia sauti za mahaba.. Nilikata nikapiga tena kwa mara ya pili ikapokelewa.. “..Aisha uko wapi, sie tunarudi kubadilisha nguo bwana..?” “..angalieni upande wa pili huku kwenye giza giza karibu na ukuta wa chuo cha ‘Dit’ kwenye kagiza mtaona gari ya bluu imepaki ndio tulipo..” Nilikata simu nakumchukuwa Lucy mpaka lilipopaki hilo gari. Sikuwa naifahamu hata kidogo, “..Aisha na yeye wachini chini..?” Nilikuwa naongea na Lucy huku tukilikaribia hilo gari, ile tunafika tu Aisha akafungua mlango kwa mbwembwe zote huku akimvuta bwana wake atoke, Nilimwangalia mara moja tu, uso kwa uso na sura niliyokuwa naifahamu sikuonesha kutetemeka wala kuogopa kwa nilichokiona, nilijikaza nakuongea kwa kujiamini huku nikisita kumpa mkono.. “..John habari yako..?”

:: Eeebwana eeeeh we unazani nini kitafuata baada ya tina kukutana na john ana kwa ana  na muda sio mrefu walitoka kuongea kwenye simu na kila mmoja alipaniki kwa mwenzie je john atamfanya nini tina baada ya kukutana nae na vipi kuhusu Aisha akigundua kama Tina ametoka kimapenzi na john na kamuambukiza virusi vya ukimwi…? Fuatana na mimi katika toleo lijalo la mkasa huu wa kusisimua…

:: usikose kufuatilia kisi hiki mpaka mwisho kwani sio ya kuikosa kabisa