MALAYA MZOEFU..03Mtunzi: JONS JONASMsimuliaji:CLIFF DAVISWhstsApp:0613 321 991Kabla sijaanza kukusimulia simulizi hii ya Malaya mzoefu sehemu ya Tatu, ningependa kukukumbusha jambo muhimu sana. Tafadhali hakikisha unasubscribe kwenye chaneli hii Ya Simulizi Extra, ili uwe wa kwanza kupata muendelezo wa simulizi hii pamoja na simulizi nyingine za kuvutia. Pia, usisahau kulike na kuacha maoni yako; maoni yako ni muhimu sana katika kutusaidia kuboresha simulizi zetu na kuhakikisha kuwa zinaendelea kukufurahisha. Kwa kufanya hivyo, utakuwa umetisha kinomanoma! Sasa bila kupoteza muda, wacha nikupeleke moja kwa moja kwenye simulizi yetu ya leo, inayomhusu mrembo Tina, ambaye alitumia mwili wake barabara kujifurahisha.Mimi ni mr.story Cliff Davis, na ni faraja yangu kubwa kukukaribisha kwenye safari hii ya kusisimua. Twende tukaendelee na simulizi hii..::
Tuliishia pale ambapo mrembo tina yupo kwenye bajaji baada ya kuondoka nyumbani kwa jerry usiku wa manane na suka wa bajaji yaani dereva anaeiendesha bajaji alikuwa anampa story fupi ya bwana jerry kuwa kazi yake ni kuchezea mabinti za watu na pia jerry ni muathirika wa virusi vya ukimwi na pia anasambaza kwa makusudi na ukishaingia kwenye anga zake ni lazima akuambukize na kisha anakufukuza nyumbani kwake…..we unafikili kinajiri twende tukaianze pamoja:: “..sasa ‘aunt’ huniamini au..?” “..embu chukuwa hela yako nishushe hapa hapa na endelea na safari yako..” Maneno makali aliyokuwa amenijaza yule dereva wa bajaj, yalikuwa yameamsha hasira zangu upya, nilimpatia hela yake akaniacha mitaa ya pale ‘Ocean road.. Nilijisogeza mpaka karibia na casino ya ‘las Vegas’ nikaingia pub moja inaitwa ‘Jolly’.. “..nipe Savvanah dry ya baridi..”Siku zote hasira zikinizidia huwa napenda kunywa pombe. Mhudumu aliniletea nikanywa, nikaongeza ya mwisho nikanywa nakumpatia hela yake. Nilivyomaliza nikaendelea kujikokota taratibu huku nikitafuta uelekeo wa chuoni kwetu. Hakukuwa na haja ya kukodi tena bajaj wala tax japokuwa zilikua nyingi pale nje huku nikiamin hata kama nitakodi yatakuwa tena yale yale aliyoniambia yule wa bajaj muda si mrefu.. Nikiwa ndio nakaribia kuingia chuoni mara simu yangu ikaita tena huku mlio ukitokea kwenye kipochi changu.. Haraka haraka nikaichukuwa nakuipokea.. “..hellow..” “..jamani Tina hivi kweli leo umeniacha hivi hivi shosti wangu..” “..yaani Aisha ni booora hata ningeondoka na wewe, kwanza hata hivyo nimeshafika hapa hostel nakuja kukupa yaliojiri huko shosti.. Nilipofika tu nilimtoa Aisha mpaka nje nakuanza kupiga naye stori usiku kucha huku nikimficha kitendo alichonifanyia Jerry na hata sikumwambia kuwa Jerry kaathirika.. “Hiyo mbon kazi ndogo tu Tina, we cha maana nipe namba yake ya simu kesho kesho atajuta kilichomtoa pemba nakuja bongo kufanya umalaya wake.., na hivi kesho wikiendi..? Mbona atapatikana tu shosti..” Alisema Aisha kwa kujidai huku akinishika mkono nakuingia ndani kulala.. *** Asubuhi na mapema Aisha alikuwa mtu wakwanza kuniamsha huku akiitaka namba ya Jerry.. Nilimpa pale pale akampigia simu, “..jamani Jerry yani mara hii umeshanisahau..? Anyway leo mie siendi kazini tunaweza kuonana..?” Aisha aliongea na Jerry kwa simu huku akijiamini kwa asilimia zote, “..shosti yangu Tina, hili limeshapatikana hapa..” “..enhe, kakwambiaje..?” “..kaniambia Jioni ya saa 12 tukutane pale ‘chaga bite’ Namanga..” Muda wote tulikuwa tunaisubiri hiyo saa 12 ifike haraka. Hatimaye ilifika na Jerry alikuwa fasta kumpigia Aisha simu, hivyo tukaenda mpaka pale na kumuacha Aisha huku mie nikijificha. Haikuchukuwa muda nikaiona gari ya Jerry, hakutaka kushuka hivyo Aisha alimfuata nakuingia ndani ya gari kisha wakaondoka. “..ninavyomjua Jerry lazima atakuwa anampeleka kwake tu..” Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiita bajaj upande wa pili fasta.. “..unaiona ile gari mbele, ifukuzie mpaka mwisho wake..” “..ile si gari ya Jerry mtata, na tena jana usiku alimfanyia visa dada mmoja nikampakiza mpaka ‘las vegas’ lakini kama atakuwa hajaambukizwa yule? Kwanza kwa Jerry huwa hapon.. Nilijikaza nakujifanya kama siyo mimi niliyepanda bajaj yake jana usiku.. “…hayo maswali mengi yanatokea wapi wee..?” Nilivyosema tu hivyo akanyamaza kimya huku akiniendesha. Mwendo wa kawaida aliokuwa akiuendesha Jerry kwenye gari lake lililokuwa mbele yetu, ilinifanya kujawa na duku duku rohoni huku nikiamini Aisha atakuwa anafanyiwa kama nilivyofanyiwa jana.. “..kama hashikwi mapaja basi atakuwa anachezewa maziwa, na Aisha anavyopendaga hivyo mhh..” Nilijikuta najiuliza mwenyewe kimya kimya huku hasira zikinizidia kwa kuendelea kuitolea macho gari ya Jerry, mpaka ilipokata kona ya kuingia kwake.. “..sasa we nishushe hapa hapa.., unanidai sh. Ngapi..?” “..elfu 3 tu itanitosha..” Nilimpa hela yake yule dereva bajaj nakuanza safari ya kuinyemelea gari ya Jerry.. Giza lilikuwa limeshaanza kutanda hivyo ikawa rahisi kutojulikana Tina mie.. Kwa namna tulivyokuwa tumepanga na Aisha nikuwa atangulie kuingia na Jerry, kisha afanye kila njia yakumchanganyia Jerry vidonge vya usingizi, iwe kwenye juici au chochote watakachokunywa na akifanikiwa anipigie simu ili niingie ndani.. Nilijificha pale karibu na geti la kuingilia kwa Jerry takribani nusu saa bila yakupigiwa simu yeyote kutoka kwa Aisha, niliogopa endapo nitapiga mie mchezo wote ungevurugika.. Muda ulizidi kuyoyoma, nilikaa kama lisaa 1 na nusu ndipo nikapata meseji kwenye simu yangu.. Kuiangalia imetokea wapi? Naliona jina limeandikwa Jerry, nilihisi vidole vinanitetemeka huku kama presha ya ajabu inaninyemelea.. “..nilijua tu Aisha kichwa box ona sasa inshu, atakuwa ameshashtuka tu Jerry..” Niliusemea moyo huku nikiifungua ile meseji kwa spidi nijue kilichoandikwa mule ndani yake.. “..KAZI IMESHAKWISHA HUKU FANYA HARAKA UKO WAPI..?” Bado nilikuwa sijielewi elewi kwa aliyoituma ile meseji, nilichokifanya nikaifuta ile meseji nakumpigia Aisha ili nipate kujua ukweli wa hii meseji.. “..enhee vipi shosti umepata meseji yangu..?” “..ipi hiyo tena..?” “..si nimekutumia hapo kwenye simu ya Jerry, we uko wapi saa hivi..?” “..nipo hapa nje karibia na geti la huyo malaya Jerry..” “..nisubirie hapo hapo nakuja kukuchukuwa..” Ndani ya dakika chache Aisha alikuja kunichukuwa huku kichwani nikijiziba kwa mtandio ili yule mlinzi asinitambue kwani jana aliniona nilivyotoka japo ilikuwa usiku sana. Tulipitiliza hadi chumbani kwa Jerry tukamkuta kalala fofofo hajielewi, “..haya jitu lako hili hapa hata halijitambui, nililipa maji haya hapa niliyoyachanganya na vidonge vya usingizi nikaona haitoshi, liliposinzia tu nikaliongeza na sindano ya usingizi hii hapa..” “..nakuaminia shosti wangu wee wa ukweli…” “…mie ndio Aisha bwana utaniambia nini nishindwe kufanya..? Ila dah Jerry ni fundi sana aisee sijapata kuona..” “..yeah Jerry anajua kweli, kwani ulimpa..?” “..anhaaa we Tina kwani una wivu..?” “..hujanijibu vizuri Aisha, inamaana Jerry umefanya nae mapenzi..?” “ndio nimefanya nae tena kavukavu.. “…Aishaaaaa..” “..Ndio tina kwani vipi..” Aisha alinijaza hasira sana, sikutaka kumwambia nilichoambiwa na watu kuhusiana nakuathirika kwa Jerry na makusudi anayofanya kwa wasichana.. Nilichokifanya nilifungua kipochi changu nakutoa viwembe.. “..Aisha huyu Jerry si anajifanya kicheche siyo..? Mie nataka nimtahiri kwa mara ya pili hapa…” “..mh aha ha ha Tina usifanye hivyo hapa chakumkomoa nikumpa chanjo nyingi kwenye dude lake hilisikupoteza muda nikaanza kuichanjachanja huku damu zikimtoka nyingi, Jerry alikuwa bado yupo usingizini muda wote huo, “mie nayakata haya madude yake tuondoke nayo Aisha..” “achana naye kwanza hapo tu alipo usingizi ukimuisha atalia sana nadhani utakuwa mwisho wa umalaya wake..” Tulipomaliza zoezi lile lakumchanja chanja Jerry sehemu zake za siri :: Tukatoka mpaka getini lakini mlinzi akatuzuia kutoka.. “..mbona mnatoka wenyewe..? Bosi Jerry yuko wapi..?” Yule mlinzi akaushikilia ufunguo wake wa getini vizuri huku anamuita bosi wake Jerry kwa sauti akienda mpaka mlangoni nakutaka kuingia…Yule mlinzi alifungua ule mlango nakuingia mpaka ndani.. “..Aisha huyu mlinzi naona hatujui vizuri enh..” Nilimwambia Aisha huku kila mmoja akipandisha nguo yake vizuri tayari kwa na kuruka ukuta japo haukuwa mrefu sana.. Ndani ya muda mchache tulikuwa nje ya geti huku tukifurahia kitendo tulichomfanyia Jerry. “..sasa shosti tukafanye shangwe wapi..?” “..hilo tu wala usihofu, we twende pale ‘nyumbani lounge’ tukaburudike na mdada Zuchu kisha turudi zetu hostel.. *** Ilituchukuwa mwendo wa kama nusu saa kwa mwendo wa bajaj huku tukifurahia kwa mbwembwe zote.. Ilipotimia mida ya saa 8 usiku Aisha alikuwa kalewa sana ila kwa upande wangu nilikuwa bado niko freshi, hivyo tukatoka nje nakukodi tena bajaj mpaka chuoni kwetu Cbe zilipo hostel. Ndani ya dakika chache tayari tulikuwepo hostel, nilimkokota Aisha wangu mpaka bwenini, tukajipumzisha japokuwa akili yangu ilikuwa haipo pale kabisa, kila muda nilitamani japo nipige simu ya Jerry nijue kama tumempa ulemavu wa maisha au limekufa kabisa.. “..naombea nisikie limekufa hata sasa hivi..” Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiuweka mto vizuri tayari kwa kulala.. Kesho yake asubuhi na mapema ambapo Aisha alikuwa bado na uchovu kalala fofofo, nilichukuwa simu yangu nakutuma meseji ya kiuchokozi kwa Jerry huku nikiamini kwa asilimia zote itajibiwa tu, niliandika hivi.. ‘..Mambo Jerry, miss u..!’ Kweli haikupita muda nikapigiwa simu.. “..hallow..” “..sorry, naongea na Jerry..?” Sauti niliosikia ni tofauti na ile ya Jerry.. “…Jerry yupo hapa Ocean road kalazwa yupo hoi toka usiku wa leo kwani we nani mwenzangu..” Nikajichekea kimya kimya na kwa dharau huku nikiendelea kumdadisi yule mtu.. “..jamani mpe pole sana sana, mchana wa leo nitakuja kumuangalia, mie ni rafiki yake naitwa Tina..” Nilipomaliza tu kuongea na simu, nilishikwa na furaha ya ajabu huku mwili ukinisisimka nakuamini alichonifanyia mara ya mwisho kwake tayari nimeshalipizia.. Ilipofika mida ya saa 5 tano tano, Aisha naye alikuwa ameshahamka hivyo nikamwelezea kila kitu, nakumwambia yeye abaki mie nitaenda huko hospital kuhakikisha.., Kwakujifanya na mie nilikuwa nampenda Jerry nikanunua Juici kubwa ya box na matunda matunda mchanganyiko, kama kawaida kichwani nikajifuka kwa mtandio huku chini nikiwa na gauni refu lenye heshima, nikiwa ndio nakaribia tu hospitali ya ‘Ocean road’ nikanyanyua simu nakupigia tena ile namba ya Jerry.. “..samahani, unaweza kunielekeza wodi aliyolazwa..?” “..njoo huku ‘block C’ wodi namba 4 single..” Nilifuata maelekezo mpaka hapo, na nilipoingia nilikutana na wasichana wengi kama 10 na, huku wakiwa wameleta vyakula mbalimbali, wanaume walikuwa wawili tu huku baadhi ya wasichana wakishindwa kujizuia nakulia kwa sauti ya juu.. Jerry bado alikuwa usingizini hivyo nilishindwa kumuona akiongea.. Yule niliyekuwa naongea naye kupitia simu ya Jerry ni ndugu yake kabisa na Jerry, nilipofika yeye ndiye alikuwa karibu yangu sana nakunipa maendeleo ya Jerry alivyoambiwa na dokta.. Nikuwa itamchukuwa muda mrefu kupona haswa lile eneo la juu ya nanii yake.. Matamanio mengine yakanianza hapo.. “..duh, Kumbe ndugu zake Jerry wazuri, dah ila sidhani kama atakuwa na tabia kama za Jerry..” Niliusemea moyo huku nikimpa vile vitu nilivyoleta. Kama kawaida Tina mie nikishaonaga wanaume weupe tu akili yote inahama nakuanza matamanio.. Nilijikaza Tina mie nakumuongelesha yule mkaka.. “…samahani naweza kukwambia kitu, mie nataka kuondoka..” “..bila samahani wala usihofu..” Alinifuata nikamtoa mpaka nje nakuanza maongezi naye.. “..najua utashtuka kukuita huku lakini nachoweza kukwambia ni kwamba…” Kabla sijamalizia kuongea, yule kaka akapigiwa simu akapokea, alivyomaliza tu kuongea na simu akanyong’onyea ghafla.. “…Ohh my God..!! Jerry hatunaye tena… Nikabaki na mshangao huku siamini amini, tukajikuta wote tunakimbia mpaka wodini kuhakikisha kama kweli Jerry kafa.. Tulipofika tu wodini wasichana walikuwa bado wamemzunguka Jerry huku wakimlilia zaidi, “..itakuwa kafa kweli nini..?” Niliusemea moyo huku nikijipenyeza katikati ya wale wasichana. Tabasamu kubwa alilokuwa analitoa ndicho kitu kilichowatoa zaidi machozi wakinadada waliokuwa wanamlilia, Jerry alikuwa hajafa japokuwa alikuwa hawezi kuongea lakini macho yake yaliweza kuangaza huku na kule.. Bado swali moja lilinisumbua kichwa, ninani aliyemwambia ndugu yake Jerry kwenye simu kama Jerry kafa..? Nilimshika tena mkono kwa mara ya pili yule ndugu yake na Jerry mpaka nje.. “..embu niambie vizuri nani aliyekwambia Jerry amekufa..?” “..anhaa, ile simu nilipigiwa na mjomba na nikweli Jerry amefariki..” “..Jerry..? Jerry gani sasa..?” “..Huyo mjomba wetu naye anamtoto anaitwa Jerry ujue jina la Jerry ni la marehemu babu yetu, sasa huyo mtoto wake mjomba alizaliwa akiwa na moyo mkubwa, na aliugua sana, ndio hivyo tena kazi ya mungu haina makosa..” “..dah, poleni sana..” Nilisisimka kana kwamba na mie ni ndugu wao tena ukarimu niliomuoneshea huyu kaka.. “..kwa hapa Dar unakaa wapi..?” “..mh, nakaa kinondoni pale ‘mkwajuni..” Alinijibu huku akinionesha tabasamu nakunifanya nisisimke tena huku nikiuangalia ‘lips’ zake mara mbili mbili jinsi zilivyokuwa pana.. “..hata kama wanamatatizo, sijui wamefiwa, sijui wanauguza, mie hilo wala silitambui, huyu Kaka kweli simuachi..” Niliusemea moyo huku nikimrembulia macho nakuvilazimisha vidimpozi vyangu feki.. “..ok, lakini unaonekana kama umeoa enh..” “..we bado umri haujafika, ndio kwanza nipo mwaka wa kwanza pale Ifm..” “..sasa hapo kinondoni unaishi na nani..?” “..pale nimeamua kupanga tu kachumba kamoja, sipendi kukaa hostel.. Wewe unakaa wapi..?” Kabla sijamjibu dokta akaja maeneo yale tulipokuwa naye nakuongozana naye mpaka ofisini.. Nilirudi kumuangalia Jerry kinafiki kujua anahali gani.. Kwa kipindi hiki alikuwa kafunga macho kuonesha kuwa anausingizi sana, nilitamani nichukuwe sindano pale pembeni yangu nakumchoma tena nanilii yake..:: Kitendo alichonifanyia Jerry cha kuniingilia kinyume na maumbile ndicho kilichoniuma sana nakumchukia Jerry kila nilipokuwa namuangalia pale kitandani.. “..na kama amenipa ukimwi, naurudisha tena kwenye ukoo wao, nitahakikisha natembea na ndugu zake mpaka nawamaliza..” Hasira kali nilizokuw nazo ilinibidi kuzipunguza kwa kutoka nje kabisa huku nikimsubiria John ‘ndugu yake Jerry’ atoke huko ofisini kwa dokta.. Haikumchukuwa muda sana nikamuona John ametoka huku akionekana mwenyehuzuni sana.. “..enhe vipi dokta kakwambiaje..?” Nilimuuliza kwa shauku ya hali ya juu.. “…Dah, ‘bro’ maendeleo yake yanatia huruma, na nikija kumjua aliyemfanyia hivyo, atanijua kama mimi natokea Pemba ama Unguja..” “..ok, niambie basi kitu gani umeambiwa na dokta..?” “..ni kwamba bro Jerry anapata shida sana kukojoa, hivyo watamfanyia upasuaji mdogo ili kupata njia nyingine yakutolea mkojo. Na vile vile kunamshipa wa uzazi nao ulichanjwa ukawa wazi hivyo anaweza akakosa uwezo wa kuzalisha tena maishani mwake..” Pale pale nikajifanya kama muvi za kibongo nikaanza kutoa machozi yakinafiki huku nikilazimisha kukohoa na makamasi kuyavuta yalioambatana na chafya bandia.. Alinibembeleza sana, lakini ni kama alinizidishia sauti, kwani nilizidisha sauti kana kwamba nimefiwa. Umati wa wauguzi pamoja na wapita njia ndio walionisaidia kuninyanyua pale chini nilipokuwa natapatapa huku nikilitaja jina la Jerry mara nyingi nyingi. John alinibeba akisaidiana na wapita njia mpaka kwenye gari ya Jerry kisha, “..unaishi wapi nikupeleke..?” Aliuliza John kwa hasira, kwani nilivyolia kwa sauti kulimkera sana, kumbe mie nilikuwa na mtego wangu.. Nikashusha pumzi huku nikijifuta machozi feki nakumuangalia John.. “..nipeleke kwako kwanza nikabadilishe nguo yangu ya ndani imechafuka sana, niko katika mwezi..” Nilimdanganya ili iwe rahisi kuwa naye lakini alionesha kama kushtuka kitu, “..lakini mbona hapa kuna vyoo na unaweza kubadilisha tu..” “..kama hutaki nishushe, kwani hapa kuna mabafu? Nataka nioge kabisa..” “..ok, mie niko tayari kukupeleka hadi kwako hata kama ni mbali.. “..naishi hostel, na leo Jumapili wanaume kibao bwenini..” Hadi mwenyewe akakubali nakuliwasha gari nakuelekea kwake, furaha ya ajabu iliyoamsha mshawasha wangu huku nikijiamini kwa asilimia zote huko tuendako lazima kieleweke tu.. Ile tunafika njia panda ya kuelekea kinondoni, John akapigiwa simu lakini hakupokea alichoniambia nipokee halafu niweke ‘laudi spika’ kwakuwa yeye anendesha gari, “..halow..” “..vipi mpenzi wangu J uko wapi? Mi niko kwako hapa…:: Wewe unafikili nini kitaendelea na tayari tina kashaamua jambo lake na anasema li lazima lifanikiwe je john na tina watafanikiwa kufika nyumbani kwa john na vipi mpenzi wa john amabe yupo nyumbani kwa john akimsubiria tina atachukua uamuzi gani atashuka njiani au atakomaa hadi kwa john na vipi kuhusu jerry kule hospitali je atapona au atafariki….usikose kufuatilia kisi hiki cha kusisimua mpaka mwisho kwani sio ya kuikosa kabisa :: USISAHAU KUSABSCRIBE,KULIKE NA KUKOMENT bila kusahau kuSHARE kwa wingi Zaidi ili iwafikie watu wengi zaidi jina langu nini ni mr story cliff davis bila kumsahau mtunzi wa simulizi hii JONS JONAS amabe anapatikana kwa namba hizi 013321991 hadi wakati mwingine katka mwendelezo huu wa kusisimua asante kwa time yako chaoo
0 Comments