NILILALA
NA MAITI 20 ILI NIOLEWE NA RAISI SEHEMU YA 3
Mtunzi: JONS JONAS
Simu: +255 613 321 991
Ilipoishia…
“Adela mwanangu umekuja?”
Aliongea yule mama wa kwanza kabisa. yule
alioniambia kuwa ni kiongozi wao na atanipangia kazi ya kulala na maiti
ishirini.
“Ndio mama”
“Umependeza mwanangu! Hivyo ndivyo mabinti
wakike wanavyoishi huku kwetu.
Si umeniona hata mimi sinma maziwa? Yaani huku
hayana kazi maana kama mimba hatupati sasa miziwa inafanya kazi gani?”
Songa nayo…
************************************
Nilijiangalia mara mbili mbili kifuani mwangu
kwa hasira ya hali ya juu.
Yale maziwa madogo dogo na ya kumvutia kila
mwanaume sasa yalikuwa hayapo tena katika kifua changu. Yametolewa na wale
wazee wachawi wenzangu.
Niliumia sana lakini kwa kuwa tayari
nilishakubaliana na nguvu ya kiuchawi ilinibidi yatolewe.
“Adela?”
“Abee mama!”
“Kuanzia sasa usiniite mama, mimi siyo mama yako
sawa?
Mbona mimi sikuiti mwanangu na kuita Adela?
Nataka uniite Sophia ama sophy, tumeelewana Adela?”
“Ndio sophy nimekuelewa.”
“Haya sogea karibu yangu hapa nilipo kisha
nikumbatie kwa nguvu.”
Aliongea yule Sophy kwa sauti ya ukali
akinisisitizia kwa mkazo.
Nilitahamaki maneno yake ya ukali lakini
nilijikuta naingiwa na moyo wa subira.
Moyo wa kuvumilia yote nionayo na nisikiayo.
Mwili wangu bado ulikuwa haujakamilika kabisa
kwa uchawi kwani nilianza kuhisi woga woga ukininyemelea kila muda niliokuwa
nikiongea na Sophy.
Hata aliponisihi nimsogelee na kumkumbatia bado
nilikuwa nikimuogopa.
“Hivi unanisikia Adela ninachokuambia? Au
unataka nikurudishe kule kwa wazee ulipokuwepo wakakuchezee tena mwili wako?”
“Hapana mama, anhh nisamehe!!. Hapana Sophy!”
Kwa uoga uliochanganyikana na aibu kwa mbali
ilinibidi nimsogelee na kisha nichukue mikono yangu na kupitisha mabegani mwake
kwa lengo la kumkumbatia kama alivyohitaji.
*******
Baridi kali lilikuwa likiendelea kuusumbua mwili
wangu. Kiza kinene kiliyashinda macho yangu angavu. Macho yenye nguvu ya
kuangaza popote sasa yakawa hafifu.
Hafifu kwa kutoweza kuona vizuri mbele wala
nyuma. Nikajikuta nikiwa juu ya mti mkubwa sana. Mti aina ya mbuyu uliopukutika
majani yake na kuwa mkavu.
Nafsi yangu iliuliza moyo lakini akili ilibaki
kutokujua na kukataa kuujibu moyo juu ya kinachoendelea.
Sauti za ndege aina ya popo na bundi ndizo
zilienea zaidi. Mwili wangu haukuwa mwili wa kawaida tena kutokana na kujikuta
nimezungushiwa shanga na hirizi karibu mwili mzima na mikononi nikiwa
nimefungwa vitambaa vyekundu.
Pembeni yangu alikuwepo Sophy akiwa amebebelea
ungo mkubwa uliokuwa umejaa vibuyu, vidole vya watoto, masikio ya watu wazima
pamoja na mikia.
Sikuelewa vizuri ilikuwa ni mikia ya mnyama gani
kutokana na mikia kuwa mirefu sana.
Sophy alionesha kufurahi jambo akinitazama usoni
mwangu.
“Adela sasa kazi yetu inaanza rasmi sasa hivi.
Na hapa nilipo nipo kwa ajili ya kukuonesha tu
utakavyokuwa unafanya na siku nyingine utakuwa unakuja peke yako mpaka
utakapomaliza zoezi la kulala na maiti zote ishirini, umenielewa Adela?”
“Nimekuelewa Sophy”
Nilijibu kwa kujiamini kana kwamba tayari ni
mchawi aliyekamilika.
Baada ya hapo Sophy akachukuwa Mikia miwili na
mmoja wapo akanikabidhi kisha akaniamuru ule mkia niwe nauchovya kwenye kibuyu
kuna nguvu zetu za kutulinda tusionekane na wala tusikamatwe na mtu yeyote na
hata tukikutana na mchawi ambaye hayupo katika himaya yetu asiweze kutudhuru.
Nilifanya hivyo pamoja na Sophy naye alikuwa
akifanya hivyo hivyo huku tukishuka kwa kuteleza chini ya mbuyu taratibu.
Tulipofika chini kabisa nilishangaa kukutana na
makaburi mengi yakiwa yamejipanga.
“Adela?”
“Abee Sophy?”
“Haya ni makaburi ya Mwananyamala na kwa kuanza
chukua hiki kibuyu kitakuwa kinakuongoza.
Unapita mstari huu wa makaburi huku ukiyapandia
juu yake mpaka kule mwisho na ukijiona mzito unashindwa kwenda mbele ujue hilo
ni kaburi la mwanaume ambaye amezikwa leo leo.
Haya tuanze mimi nipo nyuma yako taratibu”
Nilijikuta nauvaa moyo wa kijasiri na
wakiuchawi. Woga uliniyeyuka ghafla na kuvaa ngozi ya kichawi tena yule mchawi
aliyekubuhu kwa uchawi.
Nilianza kupiga hatua nikifuata mstari wa
makaburi kwa kuyakanyaga juu yake.
Nilifanya hivyo kwa zaidi ya makaburi sita
lakini nilipolikaribia kaburi la saba nilishangaa mwili wangu kama
kutetemeshwa.
Ganzi! Ndio ganzi mithili ya shoti ya umeme
ilikuwa imeninyuka katika miguu yangu vilivyo.
Nilitetemeka na kutaka kuanguka mpaka chini.
“Adela? Nini tena unafanya? “
“Sophy nashindwa kutembea, nashindwa nivute?”
“Hivi unajua kuwa ilo sio kaburi unalotakiwa
kulichimba leo. Na kaburi hilo uliokanyaga ni la zamani sana.
Ukiona miguu inatetemeshwa ujue hilo kaburi litakuwa
la mchungaji ama kiongozi wa kanisa au msikiti.
Mara nyingi huwa inatutokea tukiwa katika
mawindo yetu haya. Sasa si unaona na maua kabisa yanaonekana yamewekwa leo.
Watakuwa walikuja kulisafisha na kuliombea
mchana au asubuhi”
“Ndio”
“Lazima utakuta waliweka maji yao ya Baraka
sambamba na kuliombea lakini usijali Adela,
dawa zetu zina nguvu zaidi yao twende.”
Nilishangaa nakuwa mwepesi kwa mara nyingine.
Sophy alinivuta mkono wangu sambamba na kunipokonya kile kibuyu nilichokuwa
nacho na kubakiwa na mkia pekee.
Niliongozana naye kwa zaidi ya makaburi kumi na
moja akasimama.
“Adela umepaona hapa?”
“Ndio”
“Hapa kibuyu kimekataa kusogea na hata mkia
pamoja na shanga zangu za kiunoni nilizokuwa nazo zinacheza cheza sana. Na wewe
umehisi hilo?”
“Mimi zinaniwasha sana na mkia nilioushika
unajitingisha wenyewe.”
“Basi hapa ndipo penyewe. Kama ukiona kibuyu
kinacheza peke yake ujue hilo ni kaburi la mwanamke achana nalo.
Lakini kama utaona kibuyu pamoja na mkia na hizo
shanga ulizonazo zote zinacheza cheza ujue hilo ni la kiume na hata si unaona
kaburi lilivyo jepesi pamoja na mchanga wake uliofukiwa inaonyesha dhahiri kuna
maiti ya kiume tena imefukiwa leo leo.
Haya unatakiwa uweke kibuyu hapo pembeni ya
msalaba wao hili nguvu yetu ya kichawi iweze kushinda na baada ya hapo utatumia
mikono yako kuchimba hili kaburi.”
Ule woga wote niliokuwa nao ulishafutika toka
nimekatwa maziwa yangu na kuwa mchawi kamili.
Roho ngumu na ya kichawi ndio ilionitawala
katika halmashauri ya kichwa changu. Kwa haraka zaidi nilifanya kama
nilivyoelekezwa na Sophy.
Nilichimba kaburi kwa kutumia mikono yangu.
Nilishangaa nguvu za ajabu nilizokuwa nazo za
kuweza kulifukuwa kaburi refu kwa muda mchache, nilijikuta nimeshafika umbali
mrefu sana.
Niligeuza macho yangu kuangalia juu nilipotoka
lakini sikuweza kumuona Sophy japokuwa kulikuwa na mwanga wetu wa kichawi
uliosaidiana na mbalamwezi.
Nikaendelea na kilichonileta hapa kaburini.
Baada ya kuendelea kuchimba kwa muda kidogo nilikutana na mbao mbao.
Akili yangu ikajibizana na mdomo na kutambua
kuwa ilikuwa ni jeneza. Nilishika mbao zake kwa nguvu zote na kuanza
kulifungua.
Nilifanikiwa kulifungua japokuwa nilikutana na
harufu kali sana. Mara nyingi harufu za kichawi hufanana sana na zile pafyumu
za kupulizia maiti hivyo hazikuniathiri pua zangu ama mimi mwenyewe.
“Umependeza!!”
Nilijikuta natoa mdomo wangu nakuusemea moyo
huku nikiangalia ile maiti kwa jinsi ilivyokuwa imevalishwa suti nzuri na ya
kuvutia.
Nikalitoa bao lote lililokuwa limefunikiwa kwa
juu. Nikaanza kumvua nguo zake taaratibu kuanzia tai, koti la suti na kisha
nikamalizia suruali yake mpaka akabakiwa uchi kabisa.
Mwili wake ulikuwa umesinyaa sana nadhani
ilitokana na kukaa mochwari kwa muda mrefu ama alikuwa akiugua sana hilo sikulijali
Adela mimi zaidi ya kuendelea kumvua nguo.
“ Mlambe lambe kuanzia kifuani, mdomoni, na
kisha umnyonye sehemu zake za siri. Ukimaliza ufanye naye mapenzi kwa kumlala
juu yake kama wafanyavyo wapenda nao huko duniani!”
Sauti mbili mbili zilizochanganyikana na sauti
ya Sophy zilikuwa zikitikisa ngome ya masikio yangu.
Nikataharuki! nikaanza kuzubaa sasa. Kadiri
nilivyokuwa nikizubaa kwa kuzisikiliza sauti zile zilipotokea ndipo nazo
zilikuwa zinaongezeka na kurudia maneno yale yale.
Kwa takribani dakika tano nzima zile sauti
ziliongezeka mara kumi ya pale kwani niihisi watu wengi sana wananiambia maneno
yale.
Mwili wangu ulishtuka kama vile ulipigwa na
radi. Nilijikuta ghafla nikisisimka sambamba na furaha.
Nikaanza taratibu kulamba usoni ile maiti na
mikono yangu nikiitumia kumtoa pamba zake puani na masikioni mwake.
Niliendelea kumnyonya mdomoni mwake ulimi wangu
nikiutelezesha mpaka kifuani mwake.
Nikiwa bado katika hali ya kumnyonya ghafla
nikashangaa ile maiti kushtuka. Nikataharuki!
nikainuka na kuiangalia vizuri, nikashangaa
jicho moja la maiti hii likifumbua na kunitazama kama inataka kunisemesha
jambo.
Nikabaki nimetulia kama mtu aliyegongewa
misumari katika mbao au bati.
“Sophhhhhyyyyy??”
Uzalendo ulinishinda kabisa nikabaki nikitoa sauti
ya ukali na ya juu kabisa kumuita Sophy.
Sophy yule niliekuja naye huenda nilikosea
masharti au nguvu za kichawi zimeniishia.
Lakini sikuambulia msaada wowote zaidi ya ile
sauti nilioitoa kumuita Sophy ikinirudia mwenyewe mithili ya mwangi wa sauti katika
mapango marefu na yenye giza.
***********************
**** Unavyodhani Adela atanusurika hapo na hiyo
maiti? Vipi kuhusu Sophy?, atakuwa wapi au amerudi kule kwa wachawi wenzake
akamuacha Adela? Nini hatma ya maisha ya Adela?
**** Simulizi ndio kwanza imeanza, tegemea utamu
zaidi kila itakapokuwa inaendelea. Gonga LIKE zikifika 200 naachia tena
nyingine.
**** ANGALIZO ****
Hairuhisiwi kusoma kwa mtu ambaye anajijua ni
muoga. Ukijihisi kila unaposoma mapigo ya moyo yanakwenda kasi, tafadhali acha.
Pia si vizuri ukawa unasoma katika mazingira ambayo upo peke yako ama unaishi
peke yako katika nyumba hasa nyakati za usiku. Na siyo vizuri kusoma ukiwa
maeneo ya beach,chini ya miti mikubwa ama karibu na makaburi, hospitali zenye
vyumba vya kuhifadhia maiti ama milima ni hatari sana.
0 Comments