Story:
Nililala na maiti 20 ili niolewe na Rais - 01
Mtunzi: Jons jonas
Simu: +255 613 321 991
Machozi yangu yaliendelea kunibubujika katika
paji la uso wangu mithili ya maji yakifuata mkondo wake. Niliendelea kugalagala
chini huku nikiwa sijitambui.Kwikwi ya ajabu ilinibana sana ilioambatana na
kukohoa pasipo na mpangilio. Sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuwa
nikikishuhudia mpaka pale niliposhikwa mkono na jirani zangu niweze kumwaga
mchanga wa mwisho katika kaburi kubwa. Kaburi refu lililokuwa limechimbwa na
majirani wema kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama yangu kipendwa, mama Adela.
Mama aliokuwa ameniacha mimi mtoto pekee tangu alipofariki baba miaka mitatu
iliopita na kutuacha katika kipindi kigumu cha kutegemea milo miwili kwa siku.
“Umeniacha mkiwa mama, Niacheniii…?”
Ghafla nilitekwa na nguvu za ajabu katika mwili
wangu. Nikayatoa macho ya ukali kuwaangalia wale wakina mama waliokuwa
wamenishika. Mmoja wapo alionekana kuwa na ukali dhidi yangu. Hilo
sikulistaajabu, kwa kutumia meno yangu niliweza kuwang’ata wote wawili mikononi
mwao na ndio ukawa mwanya wa mimi kudumbukia katika kaburi la mama yangu. Kamwe
sikutaka kuyabinua macho yangu kutazama juu nilipotoka. Nguvu ya ajabu
iliendelea kunitawala katika mwili wangu, nilijikuta nikifungua lile jeneza
lililoupumzisha mwili wa marehemu mama yangu kipenzi, mama Adela pasipo woga wowote.
“Mama? Mama? Amka mama yangu japo nikuone tena
kwa mara ya mwisho mama?”
Niliendelea kulia kwa uchungu huku mikono yangu
miwili ilikuwa imeng’ang’ania uso wa mama yangu sambamba na kichwa chake
kilikaribiana kabisa na cha kwangu.
“Mama? Hutaki kuamka? Mie nitaishi na nani tena
mama yangu?”
Hasira ilinizidia mara mbili ya awali. Ilinibidi
niutoe ulimi wangu nakuudumbukiza katika mdomo wa mama yangu. Nilichukua mikono
yangu nikaisogeza mpaka masikioni mwa mama kisha nilimtoa pamba masikioni mwake
nakudumbukiza vidole vyangu. Nilivuta pumzi yangu kwa kasi nikidhani huenda
atashtuka. Kadri nilivyozidisha ndivyo na harufu kali ilikuwa ikinirudia kutoka
mdomoni mwa mama. Nilijihisi mwili wangu unabadilika kwa haraka zaidi. Ile
mikono ambayo niliitumia kumuingizia vidole masikioni mwa mama yangu sasa
ilikuwa imebadilika rangi na kuwa na maji maji mithili ya rangi ya kijani
kijani.
*******
“Hapa ni wapi? Na mama yangu yuko wapi?”
“Nyamaza na utulie kimya Adela wewe?”
Woga ulianza kunitanda kwa ghafla. Sauti kali ya
kike ilikuwa imetingisha ngome ya masikio yangu baada ya kunitaja jina
langu.Mwili wote uliendelea kulowana si kwa maji bali kwa jasho langu mwenyewe.
Sikujua sababu ilionifanya kufika katika eneo hili. Eneo lililokuwa limejaa
maajabu ya kila aina. Hakukuwa na nyumba hata moja bali watu walikuwa
wakipishana wenyewe tena walitembea wakiwa hewani. Si magari wala nyumba la
hasha! hazikuwepo. Hakuna hata mmoja aliokuwa amevaa nguo zaidi yangu japokuwa
nguo nilizovaa zilikuwa zimenichakaa kwa vumbi na damu damu lililogandia.
niljihisi mwili wote kuishiwa na nguvu sambamba na kizungu zungu huku macho
yangu yalionesha kutoshirikiana katika kumsiliza mama aliyekuwa mbele ya macho
yangu.
“Adela unakumbuka mara ya mwisho ulichokuwa
ukikifanya?”
Alirudia jina langu kiufasaha hali iliyonitia
woga mara mbili yake huku nikijiuma uma kwa kujibu.
“Hapana sikumbuki”
“Hukumbuki?”
“Ndio sikumbuki na niambieni kwani nilifanya
nini na hapa ni wapi mbona sielewi?”
“Unawaona wasichana wenzako kule na kule
wanaozunguka wakiwa uchi?”
Haraka haraka niliyazungusha macho yangu
kutazamana kinachoongelewa na huyu Mmama.
“Ndio nimewaona”
“Hawa wote hawana wazazi kama ulivyokuwa wewe na
hapa unapowaona mchana huu wote tupo nao na ikifika usiku kila mmoja anaenda
kazini”
“Kazini? Ndio wapi na ofisi gani hizo za usiku?”
“Eeeh he heee!! Embu wacha kunichekesha Adela.
Wewe ulikuwa umeshapoteza uhai ukiwa ndani ya kaburi la mama yako pindi
ulipokuwa unamlilia. Na hapa ninavyoongea na wewe si mtu hai bali ni mfu”
“Mfu? Inamaana nilishakufa nikazikwa?”
“Ndio Adela, wewe ni mfu. Mjini kote wanajua
kuwa ulishakufa toka kipindi kile ulichodumbukia katika kaburi la mama yako na
leo ni siku ya tano umezinduka hapa kwetu. Na ni sisi ndio tuliokupa nguvu za
ajabu na kuweza kuishawishi akili yako ifanye vile mpaka kufikia hatua ya
kumnyonya mama yako ndimi huku ukimdumbukiza vidole vyake katika masikio yake.
Wale wadada unaowaona kule ndio waliofanikisha zoezi zima la kufanya mpaka upo
hapa.”
“Miiimi?”
“Ndio wewe Adela na hapa ninavyokwambia wamezika
gogo tu tena pembeni ya kaburi la mama yako wakidhani wamekuzika wewe!”
Machozi ya uchungu yalianza kunitoka.
Nilijitahidi japo kurudisha kumbukumbu lakini kichwa changu kiliishiwa na uwezo
wa kufikiri kabisa. Nilijihisi macho kukosa ushirikiano. Nilitumia mikono yangu
kujipangusa machozi lakini nilistaajabu mikono yangu kuwa na damu damu.
“Adela?”
“Abee!!”
“Umeingia kwenye himaya yetu huku na ni lazima
ufuate mila na tamaduni za huku kwetu hayo mengine ya duniani yaache kama
yalivyo sawa? Huna mama huna baba wala mume na hata watoto huna hilo
tunalitambua na ndio maana siku zote tulitamani kuwa na mtu kama wewe na leo
hii upo mikononi mwetu.”
“Hapana mie nataka kurudi nilipotoka nirudisheni
tafadhali, nirudisheniii?”
Hasira zilifika kikomo lakini hazikusaidia
chochote ndani ya himaya hii. Nilijiangalia mara mbili mbili umbo langu kwa
jinsi lilivyokuwa la kuvutia. Weupe wangu uliokuwa ukiwakosesha usingizi
wanaume wengi waliokuwa wakiishi maeneo ya karibu na nyumbani Ni sasa nilikuwa
nikiushuhudia ukiharibika. nilijutia hata kwanini nilikataa kuolewa wakati
nilipokuwa nikiishi na mama. Maneno ya mara ya mwisho ya mama yangu kuwa
nitulie tu nitapata mume mwema sasa nikawa nikiyajutia nakuona dunia chungu.
Posa ambazo nilizikataa kwa wanaume zaidi ya watatu waliokuja nyumbani kutaka
kunioa ndizo ziliniongezea hasira zaidi.
“Mama nataka unirudishe duniani, nakuomba
tafadhali?”
“Unajua Adela wewe ni mwanamke ambaye karibu
kila kitu tumefanana na hata mimi nililetwa na hawa wachawi wenzangu pasipo
kujijua mpaka huku na uzuri wangu niliokuwa nao. Tena wewe una bahati sana
wamekuleta wanawake wenzako ukiwa tayari umeshakufa duniani. Mimi walinileta
wazee kabisa na siku ya kwanza nilipofika nilichezewa sana mwili wangu ikiwa ni
pamoja na kubakwa mfululizo na wazee. Kila ilipofika usiku ilinibidi ni lazima
nilalae na wazee zaidi ya kumi na tano kwa usiku mmoja. Mwanzoni nilipata sana
shida lakini kwa sasa nimezoea mwenzako na mpaka nimekuwa kiongozi wa wasichana
wote wanaoletwa huku na mimi ndio wazee wamenipa uongozi wa kuhakikisha nawapa
kazi za kufanya wasichana wapya kila inapofika usiku sambamba na kuwajaza nguvu
zetu za kichawi. Kwanza niambie upo tayari kufanya nitakayokupa kisha
nikufanyie mpango urudi duniani?”
“Ndio mama nipo tayari hata sasa hivi”
“Unatakiwa ulale na maiti ishirini huku kila
moja ukiivua na kuichezea viungo vyake vya siri ikiwa ni pamoja na kuzinyonya,
kuzilamba masikioni na midomoni kama wafanyavyo wapenzi wanaopendana huko
duniani, sawa?”
“Hapana, hilo siwezi, siwezi nibadilishie
adhabu”
“Mwanangu Adela hiyo siyo adhabu hiyo ni njia ya
wewe kurudi katika mazingira ya kawaida ili usiwe mfu tena. Adela umenielewa
mwanangu?”
***************************************
***** Je Adela atafanikiwa kukubali kulala na
maiti zote na kuzifanya kama alivyoambiwa? Nini hatma yake ya maisha?
**** Simulizi ndio kwanza imeanza, tegemea utamu
zaidi kila itakapokuwa inaendelea.
**** ANGALIZO ****
Hairuhisiwi kusoma kwa mtu ambaye anajijua ni
muoga. Ukijihisi kila unaposoma mapigo ya moyo yanakwenda kasi, tafadhali acha.
Pia si vizuri ukawa unasoma katika mazingira ambayo upo peke yako ama unaishi
peke yako katika nyumba hasa nyakati za usiku. Na siyo vizuri kusoma ukiwa
maeneo ya beach ama karibu na milima ni hatari sana.
0 Comments